BENCHI la ufundi la Simba chini ya kocha wake mkuu, Joseph Omog, raia wa Cameroon, limeweka wazi kuwa licha ya mchezo wao dhidi ya Azam FC kuhamishiwa kwenye Uwanja wa Azam Complex ambao unamilikiwa na wapinzani wao hao, lakini suala hilo halitaondoa suala la wao kupata matokeo mazuri ambayo wanayataka.
Simba, kesho Jumamosi kwa mara ya kwanza watacheza na Azam kwenye mechi ya Ligi Kuu Bara ndani ya Uwanja wa Azam Complex baada ya mchezo huo kuhamishwa kutoka Uwanja wa Uhuru ambapo ulipangwa mara ya kwanza.
Mcameroon huyo ameliambia Championi Ijumaa, kuwa hawana presha na suala hilo la kwenda kucheza Azam Complex kutokana na yeye kuujua uwanja huo kutokana na kufanya kazi miaka ya nyuma pia kwenye soka la kisasa lolote linatokea haijalishi timu inacheza kwenye uwanja gani.
“Hapana, hatuna presha ya kucheza kwenye uwanja wa wapinzani wetu hao kwa sababu tumejipanga kupata pointi na tuna wachezaji wanaoweza kulitimiza hilo, lakini kwenye soka hili la kisasa haijalishi ni wapi ambapo utakuwa unacheza kama umejiandaa vya kutosha wewe ndiye utaibuka na pointi,” alisema Mcameroon huyo.
Source :Champion
No comments:
Post a Comment