SERIKALI ya Marekani inayoongozwa na Rais Trump kupitia ubalozi wake
ulioko hapa nchini, imeeleza kusikitishwa na tukio la kushambuliwa kwa
risasi Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu.
“Marekani imesikitishwa sana kuhusu kupigwa risasi kwa Tundu Lissu,
Mbunge na Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika. Tunalaani kitendo
hiki cha kipuuzi na cha kutumia nguvu. Tunaungana na Watanzania kutoa
matumaini yetu ya dhati ili apone haraka.
———————————
The United States is deeply saddened by the shooting of Tundu Lissu,
Member of Parliament and President of the Tanganyika Law Society. We
condemn this senseless act of violence and join Tanzanians in expressing
our sincere hopes for his full and speedy recovery.” Imesema taarifa ya
Ubalozi wa Marekani nchini iliyotolewa kupitia ukurasa wake wa
Facebook.
Ubalozi huo umesema unaungana na Watanzania katika kumtakia kheri Lissu
ambaye pia ni Rais wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) ili apone
haraka.
Lissu jana Alhamisi saa sita usiku alisafirishwa kwa matibabu katika Hospitali ya Aga Khan iliyopo Nairobi, Kenya.
Awali, alipatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Dodoma baada ya
kushambuliwa. Spika wa Bunge, Job Ndugai amesema leo Ijumaa asubuhi
kuwa, Lissu alishambuliwa kwa risasi kati ya 28 hadi 32, huku tano
zikimpata mwilini.
Akitoa taarifa ya tukio hilo kwenye kikao cha Bunge, Ndugai amesema
risasi mbili zilimpata Lissu kwenye miguu, mbili tumboni na moja kwenye
mkono.
Aidha, Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Vincent Mashinji amesema kuwa
amepokea taarifa kutoka kwa Mwenyekiti wa Chama hicho, Freeman Mbowe
kuwa Tundu Lissu amezinduka leo asubuhi akiwa katika Hospitali ya
Aga-Khan jijini Nairobi nchini Kenya, kwa sasa ameshazinduka
anajitambua na anaendelea vizuri
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Author Details
olger tz ni blog ya kuhusu habari zote za ulimwenguni hapa utaelimika utaburudika na kunufaika na mambo mbalimbali ! ungana nasi kwa habari za kitaifa,kimataifa ,michezo bila ya kusahau habari za wasanii ,visa na mikasa na kadharika!!
No comments:
Post a Comment