STAA wa filamu za Bongo, Irene Uwoya ameibuka na kusema kuwa uzuri alionao unamfanya wakati mwingine ajifananishe na jini kwani uzuri wa sura yake umekuwa ukimfanya kila mtu amuangalie kitendo ambacho anakishukuru.
Akizungumza na Risasi Jumamosi Uwoya, alisema kuwa anamshukuru mama yake kwa kumpa uzuri alionao kwani kila kukicha sura yake haipotezi mvuto kama mastaa wengine.
“Kwa kweli najivunia uzuri wangu na sifa kubwa zinaenda kwa mama yangu kwa kunipa uzuri huu pia kitu kikubwa unapokuwa staa lazima uendane na kazi ambayo unaifanya kama mimi nilivyo maana kuna wakati najifananisha na jini” alisema Uwoya
No comments:
Post a Comment