Wachimbaji wawili wa dhahabu katika mgodi wa Sekenke One kitalu namba
moja wilayani Iramba wanahofiwa kufa baada ya kufukiwa na udongo.
Mgodi huo katika Kijiji cha Konkilangi kata ya Nwike tarafa Shelui mkoani Singida.
Ajali hiyo imetokea jana Jumamosi saa 7:47 usiku mgodini humo na pia imesababisha majeruhi watano.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Isaya Mbughi amesema wachimbaji
wanaohofiwa kufa ni Simon Odochi (26) maarufu kwa jina la Wamwanza
mkazi wa Jiji la Mwanza.
Mwingine ni Kashinde Nkula (27), mkazi wa Kijiji cha Mangusu wilayani Kishapu mkoani Shinyanga.
Amesema juhudi za kuwaokoa zimeanza tangu usiku wa manane na kwamba hadi
leo Jumapili saa 3:30 asubuhi wachimbaji hao walikuwa bado
hawajapatikana.
Kaimu Kamanda Mbughi amesema ajali hiyo pia imesababisha majeruhi ambao
ni Ayubu Msengi (34), mkazi wa Ntwike; Mwita Salumu (42) wa Gumanga;
Lazaro Edward (28) wa Kiomboi Soweto; Jeremi Idd (41) wa Kijiji cha
Gumanga na Jumanne Said (24) wa Kijiji cha Mgongo.
Majeruhi hao watano amesema waliokolewa na wenzao na chanzo cha ajali hiyo ni kutitia kwa udongo
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Author Details
olger tz ni blog ya kuhusu habari zote za ulimwenguni hapa utaelimika utaburudika na kunufaika na mambo mbalimbali ! ungana nasi kwa habari za kitaifa,kimataifa ,michezo bila ya kusahau habari za wasanii ,visa na mikasa na kadharika!!
No comments:
Post a Comment