Mexico tetemeko la Ardhi lauawa Watu takribani 90 - Olgertz
TANGAZA NASI HAPA

Breaking News

Home Top Ad

TANGAZA NASI HAPA

Sunday 10 September 2017

Mexico tetemeko la Ardhi lauawa Watu takribani 90

Takriban Watu 90 Wauawa Kwenye Tetemeko la Ardhi Mexico

Takriban watu 90 wameuwa kufuatia tetemeko la ardhi la uzito wa 8.1 katika vipimo vya richa nchini Mexico kwa mujibu wa maafisa.
Msemaji wa serikali alisema kuwa watu 71 walikuwa wameuawa katika jimbo lililo kusini magharibi la Oaxaca.

Mamia ya familia zimeripotiwa kushinda katika mitaa, zikihofia hatari za mitetemeko midogo.
Wanajiolojia nchini Mexico wanasema kuwa mitetemeko midogo 721 imerekodiwa tangu tetemeo kubwa la Alhamisi.

Tetemeko hilo lilikuwa la nguvu nyingi zaid kuwai kushuhudiwa nchini humo kwa karne moja.
Siku ya Ijumaa, pwani ya mashariki mwa Mexico ilikumbwa na dhoruba inayojulikana kama Katia.
Watu wawili walifariki kwenye maporoko ya udongo baada ya mvua kubwa.

No comments:

Post a Comment