Kundi la Makomando linaloundwa na wanamuziki wawili, Fred Wayne na Muki, wanaotamba na kibao chao kipya cha Anaona Gere, nusura watwangane kavukavu baada ya kubishana kuhusiana na nani mkali kati ya Diamond na Kiba.
Akizungumza na mtandao huu, Fredy Wayne alifungukia ishu hiyo kwa kusema kilichowafanya wazinguane ni yeye kuwa upande wa Mond huku mwenzake akiwa Team Kiba.
“Muki anampenda na anamshabikia Kiba, ila mimi nampenda na namshabikia Mond, sasa juzikati tumeanza kubishana kidogo tutwangane makonde, ila baadaye tulielewana,” amesema Fredy Wayne.
No comments:
Post a Comment