TOFAUTI na mila na desturi za Kiafrika kwa mwanaume kumuoa mwanamke, mrembo Jacqueline Wolper amevunja ukimya kwa kusema, yuko tayari kumuoa ‘benten’ wake anayejulikana kwa jina la Brown.
Wolper alisema Wabongo wengi wamezoea kuona mwanaume ndiyo anatoa mahari na kuoa jambo ambalo kwake anaona ni utaratibu na uamuzi tu, si dhambi mwanamke kumlipia mahari mwanaume.
“Unajua watu wengi wanachukulia mahari ni lazima atoe mwanaume kitu ambacho siyo sahihi kabisa maana hata India siku zote mwanamke ndiyo anatoa mahari na mimi nataka kuanzisha hivyo Bongo.
Wolper.
“Najua katika hili, watu wengi wataanza manenomaneno kuwa mimi ndiyo nimeoa lakini sitajali,” alisema Wolper.
Staa huyo aliendelea kutiririka kuwa, kwenye maisha yake anapenda kuwa na furaha na kwa kuwa Brown anampa furaha ya kweli, atamlipia mahari ili kukamilisha furaha yake.
“Ninapokuwa na Brown, nakuwa na furaha sana, moyo wangu pia unajaa amani hivyo basi nahitaji kuona furaha hiyo inaendelea ndani ya moyo wangu ndiyo maana nahitaji kuwa naye muda mrefu, nimtolee mahari, tuishi na hata tuzae watoto ndiyo kitu kikubwa ninachokihitaji,” alisema Wolper.
No comments:
Post a Comment