Mourinho asubuhi ya leo saa nne tayari alikuwa amewasili katika mahakama mjini Madrid katika eneo liitwalo Puzuelo Del Alacron tayari kusikiliza hukumu ya kosa hilo alilotenda wakiwa akiwa Real Madrid.
Kesi ya Jose Mourinho ilikuwepo tangu mwezi wa sita mwaka huu akidaiwa kwamba alikuwa akikwepa baadhi ya masuala ya kodi katika kipindi cha mwaka 2011 hadi 2013.
Hii sio mara ya kwanza kwa wanasoka katika ligi kuu La Liga kukumbwa na kashfa za ukwepaji kodi kwani Angel Di Maria, Lioneil Messi, Cristiano Ronaldo na Javier Mascherano wameshakumbwa na kesi za namna hii.
Baada ya kesi hiyo sasa Mourinho anapakia ndege kurudi nchini Uingereza kuiandaa timu kwa ajili ya pambano kubwa na gumu siku ya Jumapili zidi ya Chelsea
No comments:
Post a Comment