Rais wa Marekani
Donald Trump ameishutumu ripoti iliofichuliwa kinyume cha sheria kwamba
mwanasheria wake mkuu alijadili maswala ya kampeni na mjumbe mmoja wa
Urusi.
Gazeti la Washington Post lilitoa maelezo kuhusu mikutano
ambayo mwanasheria mkuu Jeff Sessions alifanya na balozi wa Urusi nchini
Marekani Sergey Kislyak.Bwana Sessions awali alikuwa amekana kufanya mazungumzo hayo kuhusu kampeni.
Mamlaka ya Marekani inachunguza kuhusu hatua ya Urusi kuingilia kati uchaguzi huo.
- Trump ajutia kumteua mwanasheria mkuu Jeff Sessions
- Donald Trump amfuta kazi mwanasheria mkuu
- Maseneta wamuidhinisha mwanasheria mkuu wa Trump
Urusi imekana na Trump anasema kuwa kampeni yake haikushirikiana na Urusi.
Mmoja ya wale walionukuliwa anasema kuwa bwana Kislyak alizungumza na Sessions kuhusu maswala muhimu ya kampeni ikiwemo msimamo wa Trump kuhusu sera muhimu za Urusi.
Wakati alipothibitishwa mapema mwaka huu, bwana Sessions alisema kuwa hajawasiliana na Urusi wakati wa kampeni za uchaguzi.
Wakati ilipobainika aliwasiliana alisema kuwa swala la kampeni halikuangaziwa katika mkutano huo.
No comments:
Post a Comment