Bingwa mpya wa Scrabble duniani atawazwa baada ya kuandika 'carrels'
Bingwa mpya wa
mchezo wa kuunda maneno kwa kutumia herufi maarufu kama Scrabble
ametawazwa baada ya kusaidiwa na ufahamu wake kuhusu samani.
David
Eldar, 27, alishinda taji hilo baada ya kuandika "carrels" - aina ya
chumba kidogo chenye meza, sana ambavyo hupatikana kwenye maktaba katika
vyuo vikuu kumuwezesha mtu kusoma vitabu akiwa faraghani.Neno hilo lilimzolea Eldar alama 74.
Eldar alimshinda mpinzani wake Harshan Lamabadusurilya 3-0 katika fainali iliyokuwa na michuano mitano.
Tuzo ya Eldar ilikuwa pamoja na hundi ya £7,000.
Mzaliwa huyo wa Australia aliwashinda wapinzani wengine kutoka mataifa 26 yakiwemo Pakistan na Sierra Leone, kushinda taji hilo katika mashindano hayo yaliyoandaliwa Nottingham nchini Uingereza.
Mshindi huo anasema amekuwa akicheza mchezo huo kwa miaka 14 sasa na hufanya kazi katika biashara na uuzaji na ukodishaji wa nyumba na vipande vya ardhi jijini London
No comments:
Post a Comment