Wasiwasi Afrika Kusini baada ya visa vya ulaji wa nyama ya binadamu
Hofu imekumba
kijiji cha Shayamoya katika jimbo la KwaZulu Natal nchini Afrika Kusini,
baada ya kupatikana kwa maiti ya binadamu iliyonyofolewa myama yote.
Familia
ya Zanele Hlatshwayo, mwenye umri wa miaka 25, ambaye ametoweka tangu
mwezi Julai mwaka huu, ikiaminika kuwa ni mhasiriwa wa genge la watu
wanaotuhumiwa kula nyama ya binadamu, ambapo tayari washukiwwa watano
wamekamatwa.Mwili wa mwanamke huyo ambo ulikuwa umeoza, ulipatikana baada ya mwanamume mmoja kudai kuwa mganga wa kienyeji, kuamua kujisalimisha kwa polisi juma lililopita, na kukiri kuwa amechoka kula nyama ya binadamu.
Polisi nchini Afrika kusiri awali walipuuza taarifa hiyo.
Waliamua kukubali taarifa hiyo baada ya mtu huyo kutoa mkono na mguu wa binadamu uliojaa damu kama ushahidi, hapo ndipo alipokamatwa mara moja na maafisa wa polisi.
Aliwaongoza hadi katika nyumba ya kukodishwa, ambapo polisi walipata masikio 8 ya binadamu, ndani ya chungu cha kupikia.
Inaaminika kuwa zingetumika kuwalisha wateja wakeambao wanaaambiwa yana nguvu za miujiza ya kumpa mtu pesa, nguvu na ulinzi wa kutosha.
Viungo vingine kadhaa vya mwili wa binadamu vilipatikana ndani ya mkoba.
No comments:
Post a Comment