Amefanya hivyo mahakamani ambako kulikuwa na pingamizi la ushindi wa Uhuru Kenyatta,
Swali langu hivi kweli umahiri au uimara wa wanasheria wetu unafikia wa wakenya?
Niwe mkweli kwa ninachokiamini, Tanzania kila jambo limechanganywa na siasa, ndo maana hata weledi Hakuna.
Kwa wanaojua lugha ya kiingereza pitia video hii. Pia uwe na kamusi pembeni maana English ya PLO Lumumba haijawahi acha vichwa salama.
Maelezo kwa kifupi ya Prof Lumumba ni haya baadhi
1. Wamefungua kesi bila kuwa na hoja ya msingi iliyosababisha kesi kufunguliwa.
2. Affidavit badala ya kuwa nafsi ya kwanza umoja kwa mujibu wa sheria, yao inaonesha ni nafsi ya kwanza wingi. Haina mdai inshort.
3. Wamewasilisha hoja zenye takwimu na zenye mantiki, lkn wanaitaka mahakama ijikite kutoa uamuzi kwa kuzingatia maneno matupu(mantiki) na siyo takwimu ambazo zinaonesha odinga kapigwa.
4. Nasa walitangazia umma kuwa hata wakishindwa hawataenda mahakamani maana hawaiamini, leo wameenda kwenye mahakama ambayo wameshautangazia umma kuwa haitendi haki. Prejudice!
5. Wamefungua kesi wakidai aliyefungua kesi ni wananchi wa Kenya, wakati wananchi wa kenya walishapiga kura na kumpa ushindi mnono Uhuru. Sasa waliompa ushindi Uhuru, wanaanzaje tena kuupinga? Inaonesha siyo wakenye, bali ni kikundi cha baadhi ya wakenya wasioheshimu mchakato wa democrasia.
No comments:
Post a Comment