MBUNGE wa Bunda Mjini, Ester Amos Bulaya (Chadema) amelazwa katika
Hospitali ya Wilaya ya Tarime mkoani Mara usiku wa kuamkia leo baada ya
kuugua ghafla akiwa rumande ambako alikuwa ameshikiliwa na Jeshi la
Polisi Kanda ya Tarime Rorya baada ya kumkamata akiwa hotelini kwa madai
ya kutaka kufanya mkusanyiko usio halali.
Taarifa za kulazwa kwa Bulaya zimethibitishwa na Katibu wa Mbunge Tarime
Vijijini, John Heche (Chadema), Mrimi Zabron ambaye ameeleza kuwa
Bulaya anasumbuliwa na kifua ambacho kimesababisha ashindwe kuzungumza
lakini hata hivyo madaktari wanaendelea kumtibu.
Aidha imeelezwa kuwa, Bulaya alianguka na kupoteza fahamu akiwa rumande hivyo kukimbizwa hospitali kwa matibabu
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Author Details
olger tz ni blog ya kuhusu habari zote za ulimwenguni hapa utaelimika utaburudika na kunufaika na mambo mbalimbali ! ungana nasi kwa habari za kitaifa,kimataifa ,michezo bila ya kusahau habari za wasanii ,visa na mikasa na kadharika!!
No comments:
Post a Comment