Hospitali ya Muhimbili Yazindua huduma Mpya ya Malipo ili kuondoa Adha ya Foleni - Olgertz
TANGAZA NASI HAPA

Breaking News

Home Top Ad

TANGAZA NASI HAPA

Thursday, 31 August 2017

Hospitali ya Muhimbili Yazindua huduma Mpya ya Malipo ili kuondoa Adha ya Foleni

Hospitali ya Muhimbili Yazindua Uduma ya Malipo Kwa Njia ya Kielectroniki

Uongozi wa hospitali ya Muhimbili kupitia kwa mkurugenzi mtendaji wa hospitali hiyo Profesa Lawrence Maseru, amezindua mfumo mpya wa malipo ya matibabu kwa njia ya kielektroniki mapema leo mchana katika hosptali hiyo.
hosptali ya Muhimbili

Akizungumza na waandishi wa habari, profesa Maseru amesema, lengo la kusimikwa kwa mfumo huo katika hospitali ya Muhimibili ni kuondoa adha kwa wagonjwa au ndugu mbalimbali wa wagonjwa kwa kukaa muda mrefu kwenye foleni za kulipia huduma mbalimbali zinazo tolewa na hosptali hiyo.

“Dhumuni la kuja na mfumo huu kwanza kuondoa kadhia na lapsha zilizokuwepo wakati ndugu wa wagonjwa walipokuwa wakifanya malipo ya huduma mabalimbali zitolewazo na hosptali yetu. Vilevile ni kudhibiti mapato ya serilikali ambayo inawezekana kwa njia moja ama nyingine yalikuwa yakipotea,” alisema Masaju.
hosptali ya Muhimbili

Akitoa ufafanuzi namna wateja watakavyoweza kutumia mfumo huo, mkurugenzi wa fedha na mipango wa hosptali ya muhimbili Gerladi Jeremih amesema, kutakuwa na matumizi ya kadi maalumu(Muhimbili card) na kupitia mitandao mbalimbali ya simu kama Mpesa, Tigo Pesa Aitel Money nk.
“Wateja wetu watatumia kadi maalumu ambayo ataipata kutoka kwa mawakala wa Maxcom ambapo atatakiwa kujaza fedha, kisha ataelekea kwenye eneo la kulipia gharama zake za matibabu, huko atapewa mashine maalumu ambayo akipachika kadi hiyo , kiasi anachodaiwa kitakatwa na atapata risiti yake.

“Hivyo hivyo kwa watakao hitaji kulipia kwa njia mitandao ya simu, anachotakiwa kufanya ni kuchukua bili yako ya malipo na kupiga ‘menu’ ya kulipia pesa kisha unachagua kipengele cha lipa bili halafu unafuata maelekezo,” alisema Jeremiah

No comments:

Post a Comment