Madee
Msanii wa Bongo Flava kutoka Tip Top Connection, Madee amedai hakuwahi kuwa na tatizo na Afande Sele kama ilivyokuwa ikisemekana.
Madee ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma yake mpya ‘Sikila’ ambayo amemshirikisha Tekno kutoka Nigeria amesema kilichokuwa kinatokea kati yao ni kugongana kwa mashairi.
“Hamna tatizo, kwani kulikuwa na tatizo, matatizo yalikuwa kwenye mashairi ndio yalikuwa yanasuguana. Hatujawahi kuwa na mataizo mashairi ndio yana mataizo yanapokutana huko redioni lakini tukikutana bro vipi na ni mtu muhimu sana kwangu,” amesema Madee.
“Nimemuangalia kuna vitu vingi sana nimejifunza kupitia yeye. Hivi vitu vilikuwa vinazungumzwa na watu tu, watu ndio huwa wanatengeneza haya mambo,” ameiambia Bongo5.
Kwenye wimbo wa Madee, ‘Nisikilize’ Madee aliwahikusema ‘yule mkulima alidai eti namgeza, alitamba zamani miaka hii hajaweza, anaumia kwanini mwanzo alicheza, hawezi kuosha nywele ana uhaba wa fedha’.
Pia katika wimbo wa Afande Sele ‘Kingdom’ kuna mstari unasema ‘hip hop itakulipa vipi wakati unaimba matusi, unatukana ma-ras, unadiss waasisi halafu bado unadiriki kujiita rais wakati huna hata ofisi labda ni rais wa huko kwenu uwanja wa fisi’ afande sele
No comments:
Post a Comment