Jeshi la Iraq lakabiliana vikali na IS mjini Tal Afar - Olgertz
TANGAZA NASI HAPA

Breaking News

Home Top Ad

TANGAZA NASI HAPA

Sunday 27 August 2017

Jeshi la Iraq lakabiliana vikali na IS mjini Tal Afar

Baada ya wiki moja ya mapigano makali, jenerali mkuu anayeongoza oparesheni hiyo, anasema kuwa, kwa mara nyingine tena bendera ya taifa la Iraq inapepea katika eneo la Citadel.
Lakini Jenerali Abdulamir Yarallah, anakiri kuwa mapigano makali sasa yanashuhudiwa viungani mwa maeneo ya kaskazini mwa mji huoSiku ya Ijumaa maeneo muhimu ya Islamic State mjini Tal Afar yalishambuliwa na ndege za kivita za jeshi la IraqMwaandishi wa BBC, anasema kuwa, serikali ya Iraq, inatarajia kutangaza ushindi wake wa mwisho wa kuutwa mji huo, katika kipindi cha siku kadhaa zijazo.
Mji Tal Afar unatajwa kama ngome ya mwisho ya I-S nchini Iraq, lakini wanajihadi hao wangali wakidhibiti maeneo yote mawili ya mpakani, kati ya Iraq na Syria, na maeneo ya Hawija -- mji ulioko kati ya Mosul na mji mkuu wa Iraqi, Baghdad.

No comments:

Post a Comment