Wananchi nchini Kenya wameanza kupiga kura katika Uchaguzi Mkuu, wengi
wakiwa wamewasili kwenye vituo vya kupigia kura usiku wa manane.
Kwenye kituo cha Shule ya Msingi Mutomo ambako Rais Uhuru Kenyatta
atapiga kura watu wamefika hapo tangu saa kumi alfajiri.
Pia, kwenye kituo hicho cha Mutomo watu walikuwa wanafanya maombi huku
wakiwashirikisha maofisa wa Tume ya Uchaguzi isiyokuwa na mipaka (IEBC)
wa kituo hicho kuombea uchaguzi wa amani.
Kwenye kituo cha kupiga kura kilichopo Embakasi Social Hall kwenye jimbo
la Embakasi East watu walikuwapo hapo tangu saa tisa usiku na kwa
mujibu wa mwandishi wetu aliyeko Kenya Noor Shija anasema foleni hiyo
ilikuwa ndefu umbali wa kiasi cha kilomita tatu.
Maeneo mengine ambayo watu wameamka usiku ni Mombasa, Naivasha na
Nairobi kwenye kituo cha Shule ya Msingi Kahawa ambako tangu saa kumi
Watu wamejazana wakati muda wa kufungua vituo ni saa kumi na mbili.
Maeneo mengine imeelezwa vijana walikuwa wakizunguka mitaani wakipuliza
mavuvuzela kuamsha watu wakapige kura.
Kwa upande wa Nasa ratiba ya upigaji kura kwa wagombea wao ambapo Raila
Odinga atapiga kura Shule ya Msingi Olympic saa nne na nusu asubuhi
Kalonzo Musyoka atapiga kura Shule ya Msingi Tseikuru saa nne asubuhi
Musalia Mudavadi atapiga kura kituo cha Shule ya Msingi Chemakanga saa tatu asubuh
Tuesday, 8 August 2017
Kenya Waanza Kupiga Kura, Wadamka Usiku wa Manane
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Author Details
olger tz ni blog ya kuhusu habari zote za ulimwenguni hapa utaelimika utaburudika na kunufaika na mambo mbalimbali ! ungana nasi kwa habari za kitaifa,kimataifa ,michezo bila ya kusahau habari za wasanii ,visa na mikasa na kadharika!!
No comments:
Post a Comment