Wiki iliyopita Korea Kaskazini ilionekana kulegeza kamba baada ya kutisha kuwa itarusha makombora kwenda kisiwa cha Marekani cha Guam, lakini tena ikasema kuwa itafuatilia mienendo ya Marekani.
Korea Kaskazini tayari imelaani mazoezi hayo ikisema kuwa hatua hiyo ni sawa na kumwaga mafuta kwenye moto.
China na Urusi mwezi Julai zilipendekeza kusitishwa mazoezi ya kijeshi
ili nayo Korea Kaskazini iache kuyafanyia majaribio makombora.
Marekani inasema kuwa mazoezi hayo yatawahusisha wanajeshi 17,500 wa Marekani na yatadumu kwa kipindi cha siku kumi
Marekani na Korea Kusini hufanya mazoezi ya kijeshi mara mbili kwa mwaka
yanayowashirikisha idadi kubwa ya wanajeshi na zana za kivita.
Mazoezi hayo hujumuisha ya ardhini , baharini na angani. Mazoezi hayo
ambayo hufanyika Korea Kusini pia hujumuisha mafunzo jinsi ya
kukabiliana na ugaidi na mashambulizi ya kemikali
Korea Kusini hutuma wanajeshi 50,000 huku Marekani nayo ikituma kati ya wanajeshi 25,000 na 30,000.
No comments:
Post a Comment