man city wanalipwa zaidi ya milioni 650 wanaonekana kutembelea magari ya million 14 - Olgertz
TANGAZA NASI HAPA

Breaking News

Home Top Ad

TANGAZA NASI HAPA

Friday 25 August 2017

man city wanalipwa zaidi ya milioni 650 wanaonekana kutembelea magari ya million 14


Mastaa wa soka wa Man City Kyle Walker na John Stones ambao wanalipwa mishahara mikubwa ndani ya Man City leo wameonekana wakienda mazoezini na gari ndogo, thamani yake inatajwa kufikia pound 5000 ambazo ni zaidi ya milioni 14.
Kyler Walker
Kyler Walker analipwa mshahara wa pound 130000 kwa wiki ambazo ni zaidi ya Tsh milioni 370 wakati John Stones analipwa mshahara wa pound 100000 ambazo ni zaidi ya Tsh milioni 288, Stones na Walker leo wameonekana wakitembelea gari yenye gharama ndogo.

Licha ya mastaa hao kuwa na uwezo wa kumiliki gari aina yoyote ambayo mioyo yao itapenda kutumia, John Stones alionekana akimuendesha Kyler Walker katika gari hiyo na kuelekea mazoezini wakiwa wanafuraha, kitendo hicho kimewafanya waingie kwenye headlines kwa sababu haijazoeleka kuona mastaa kama wao kutembelea gari za bei ndogo.
John Stones
Kwa pamoja Walker na Stones wanalipwa pound 230,000/= ambazo ni zaidi ya milioni 650 za kitanzania, mshahara ambao kila mmoja anaweza kununua aina yoyote ya gari, sema wameamua kutembelea gari ya kawaida.








No comments:

Post a Comment