Wakati mashabiki wa Arsenal wakiendelea kujiuliza kuhusiana na hatma ya staa wao Alex Sanchez kama ataondoka au la, huku Chelsea wakiwa wameafikiana bei na Arsenal kuhusu kumsajili Alex Chamberlain kwa dau linalotajwa kufikia pound milioni 35.
Leo August 30 2017 beki wao Kieran Gibbs aliyecheza kwa mismu kumi ndani ya club ya Arsenal ameuzwa kwa pound milioni 7 kutoka Arsenal na kujiunga na West Bromwich Albion, beki huyo amejiunga na West Bromwich Albion kwa mkataba wa miaka minne.
Kieran Gibbs anaondoka Arsenal baada ya kucheza timu ya wakubwa kwa miaka kumi toka apandishwe mwaka 2007 kutoka timu za Arsenal ya vijana, Gibss hadi anaondoka Arsenal ameshinda mataji matatu ya FA, Community Shield mawili na amefunga jumla ya magoli 6 katika mechi 230 alizoichezea Arsenal.
No comments:
Post a Comment