pichani yusuph manji kabla akiwa na Afya yake
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKIC), Prof.
Mohammed Janab ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo August 30,
2017 kuwa moyo wa Mfanyiabiashara Yusuf Manji umewekwa vyuma ili
kumsaidia kupumua.
Prof. Janab ambaye ni Daktari wa moyo na Shahidi wa kwanza upande wa
uetetezi ameyasema hayo mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Cyprian Mkeha
wakati akitoa ushahidi katika kesi ya dawa za kulevya inayomkabili Manji
ambapo akiongozwa na Wakili wa utetezi, Hajra Mungula, alisema yeye ni
Daktari wa moyo wa Taasisi ya JKIC.
Amesema anamfahamu Manji baada ya kufikishwa katika Taasisi hiyo
February 2017 akiwa mwenye matatizo ya moyo na kuongeza kuwa
alipofikishwa hapo alifanyiwa vipimo na jopo la madaktari lililobaini
Moyo wake umewekewa vyuma ambapo akaingizwa mipira maalum na kubaini
kwamba upo katika hali nzuri.
”July 2017 alirudishwa tena katika Taasisi yetu akiwa na tatizo hilo la
moyo pamoja na maumivu ya mgongo na kutokuwa na usingizi.”
Prof. Janab amesema alivyorudi hapo walimpokea kama mgonjwa aliyetibiwa
nje ya nchi na ripoti ilionyesha ametibiwa Florida, Marekani.
Alipoulizwa na Wakili Mungula kama mgonjwa aliyewekewa vyuma katika moyo
anaweza kutumia dawa za kulevya, Prof. Janab alijibu kwamba huwa
haruhusiwi kufanya baadhi ya mambo ikiwemo kuvuta sigara, kutumia
Heroin.>>>”Hivyo kama akitumia athari zake ni kwamba mirija ya
moyo itaziba, kisha atatakiwa afanyiwe upasuaji mkubwa zaidi.”
Prof. Janab ameongeza kuwa katika awamu ya pili ya Manji kurudi
hospitalini hapo walimsaidia kumtibia maumivu aliyokuwa nayo kwa kumpa
Drip ya Paracetamol’s na Sindano ya Tram a do.
Akijibu hoya ya Wakili wa Serikali, Timony Vitalis kwamba matumizi ya
dawa za kulevya yanaweza kusababisha ugonjwa wa moyo, Prof. Janab
alijibu ndio.
Kesi imeahirishwa hadi August 31, 2017 kwa ajili ya kuendelea na ushahidi
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Author Details
olger tz ni blog ya kuhusu habari zote za ulimwenguni hapa utaelimika utaburudika na kunufaika na mambo mbalimbali ! ungana nasi kwa habari za kitaifa,kimataifa ,michezo bila ya kusahau habari za wasanii ,visa na mikasa na kadharika!!
No comments:
Post a Comment