Soko la Sido Mkoani Mbeya limetetekea kwa moto usiku wa kuamkia leo na
kutekteza mali mbalimbali ambazo thamani yake wala chanzo cha moto huo
mpaka sasa hazijafahamika.
Akithibitisha kutokea kwa moto huo Mkuu wa Wilaya ya Mbeya William
Ntinika amesema kuwa moto huo ambao uliwaka mpaka saa saba za usiku
ulikuwa mkubwa na kuteketeza mali zote katika eneo la kuuzia vyakula.
Ntinika amesema kuwa jitihada mbalimbali zilifanyikaka katika kudhibiti
moto huo bila kuzaa matunda ikiwani ni pamoja na kikokisi cha zima moto,
Jkt, pamoja na magari ya zima moto ya kiwanda cha Songwe lakini moto
ulikua mkubwa zaidi wakati ukiendelea kuwaka.
Mkuu huyo wa Wilaya amesema kuwa anataraji kamati ya Ulinzi na Usalama
ya Mkoa na pamoja na wilaya kukutana hii leo kwa ajili ya kufanya
tathmini na kuunda tume itakaoyochunguza chanzo cha ajali hiyo
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Author Details
olger tz ni blog ya kuhusu habari zote za ulimwenguni hapa utaelimika utaburudika na kunufaika na mambo mbalimbali ! ungana nasi kwa habari za kitaifa,kimataifa ,michezo bila ya kusahau habari za wasanii ,visa na mikasa na kadharika!!
No comments:
Post a Comment