Aliyekuwa mgombea wa Ubunge Igembe Kusini nchini Kenya, John Mwirigi
(24) ameshinda nafasi hiyo baada ya matokeo kutangazwa na Tume huru ya
Uchaguzi na Mipaka (IEBC).
Mwirigi ambaye anatajwa kuwa Mbunge mwenye umri mdogo kuwahi kutokea
aliwashangaza wengi katika kampeni zake ambapo alikuwa akitumia baiskeli
na bodaboda.
Mwirigi ambaye ni mwanafunzi wa Shahada ya elimu katika chuo cha Mount
Kenya alikuwa mgombea binafsi hakuwahi kuwa na matangazo kwa kile
kilichodaiwa kukosa pesa za kufanya kazi hiyo.
Katika matokeo hayo, Mwirigi alipata kura 18,867 huku mgombea wa Jubilee, Rufus Miriti akipata kura 15,411.
Thursday, 10 August 2017
Mwanafunzi kenya ashinda Ubunge alikua akifinya kampen Kwa Baiskeli na Boda Boda
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Author Details
olger tz ni blog ya kuhusu habari zote za ulimwenguni hapa utaelimika utaburudika na kunufaika na mambo mbalimbali ! ungana nasi kwa habari za kitaifa,kimataifa ,michezo bila ya kusahau habari za wasanii ,visa na mikasa na kadharika!!
No comments:
Post a Comment