wachina wadaiwa kupiga dili nzito kibaha katika mradi wa standi mpya mpya ya mabasi - Olgertz
TANGAZA NASI HAPA

Breaking News

Home Top Ad

TANGAZA NASI HAPA

Saturday 26 August 2017

wachina wadaiwa kupiga dili nzito kibaha katika mradi wa standi mpya mpya ya mabasi

 
Wananchi wa Mji wa Kibaha Mkoani pwani wameilalamikia kampuni ya M/S Group Six LTD inayojenga Stendi mpya ya mabasi kuwauzia kifusi cha mchanga ambacho halmashauri ya mji huo ilitoa bure kwa wananchi ili kupisha ujenzi wa kituo hicho.

Kwamujibu wa mwananchi aliyejitambulisha kwa jina la Rashid Kajumbo kutoka kampuni mzawa wa MEG Business Solution ameeleza kuwa Wachina hao wamekuwa wakiwatoza kiasi cha shilingi Elfu 5,000 hadi elfu 20,000 ili kupata kifusi hicho jambo ambalo ni kinyume cha Agizo la mkurugenzi wa  Halmashauri ya Mji wa Kibaha

Hata hivyo Rashid ambaye tayari alikuwa na kibali cha mkurugenzi mkononi cha kupewa kifusi hicho bure amesema magari yake manne yaliyo katika eneo la mradi wa Stendi hiyo inayojengwa karibu na Karakana ya Serikali hato yaondoa mpaka Waziri Mkuu Kasimu Majaliwa atakapofika katika eneo hilo na kuelezwa jambo hilo.

Baada ya madai hayo Mtandao huu umemtafuta Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Kibaha Bi.Jenifa Omolo kwa njia ya simu ambaye amesisitiza hafahamu chochote kuhusu hilo ingawa anatambua kifusi hicho kinatakiwa kutolewa bure na hivyo amefahamisha kuwa anafuatilia kama Kampuni hiyo inawauzia wananchi kifusi hicho.

No comments:

Post a Comment