Ukistaajabu ya Musa utayaona ya Firauni! Ikiwa ni miezi mitatu sasa
tangu kufariki dunia kwa mfanyabiashara maarufu nchini Uganda, Ivan
Ssemwanga ‘Ivan Don’, ambaye alikuwa mume na mzazi mwenza wa Zarinah
Hassan ‘Zari The Boss Lady’, akaunti yake ya Instagram imezua taharuki
kutokana na picha iliyopostiwa ya watoto wake, wakati dunia nzima ikijua
kwamba mmiliki wa akaunti hiyo ni marehemu.
ISHU YA KUFEKI KIFO YAIBUKA UPYA!
Baada ya picha hiyo kusambaa mitandaoni ndipo ikaibua upya lile sakata
lililwahi kuvuma kipindi cha msiba wake, kwamba amefeki kifo kwa ajili
ya maslahi yake binafsi, mpaka likasababisha polisi wa kimataifa nchini
Uganda, Interpol kutangaza kufukua kaburi lake.
Lakini muda mfupi baada ya picha hiyo, kupitia akaunti hiyo, yakatolewa
maelezo yanayomaanisha kwamba akaunti hiyo kwa sasa, inamilikiwa na mtu
mwingine, japo haikufafanuliwa kama ni ndugu yake au mmoja kati ya
marafiki zake kutoka kwenye Kundi la Rich Gang, alilokuwa akiliongoza.
TUJIKUMBUSHE KIDOGO
Marehemu Ivan Don ni raia wa Uganda, alizaliwa Disemba 12, 1977, mwaka
2002 alihamia Afrika Kusini, alipata umaarufu mkubwa kupitia uwekezaji
wake ambapo alifungua vyuo katika miji mitatu ya Afrika Kusini, kutokana
na uwekezaji huo alikuwa akiingiza zaidi ya shilingi milioni 700 kwa
mwezi.
Marehemu Ivan alipata shambulio la moyo na ndiyo tatizo hasa
lililosababisha kifo chake, usiku wa kuamkia Mei 25, 2017 akiwa katika
Hospitali ya Steve Biko iliyopo Pretoria nchini Afrika Kusini.
Alifunga ndoa na Zari, wakafanikiwa kupata watoto wa kiume watatu, Raphael, Pinto na Quincy.
Monday, 11 September 2017
Account ya Marehemu Don Ivan yazua Taharuki Instagram
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Author Details
olger tz ni blog ya kuhusu habari zote za ulimwenguni hapa utaelimika utaburudika na kunufaika na mambo mbalimbali ! ungana nasi kwa habari za kitaifa,kimataifa ,michezo bila ya kusahau habari za wasanii ,visa na mikasa na kadharika!!
No comments:
Post a Comment