Mwanasheria
Mkuu wa Chama ambaye pia ni Mnadhimu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni
na Mbunge wa Singida Mashariki, Mhe. Tundu Antipus Lissu.
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimepokea kwa mshtuko
mkubwa taarifa ya kupigwa risasi Mwanasheria Mkuu wa Chama ambaye pia ni
Mnadhimu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni na Mbunge wa Singida
Mashariki, Mhe. Tundu Antipus Lissu baada ya kikao cha Bunge mchana wa
leo.
Shambulio hilo limetokea majira ya mchana nyumbani kwake Area D
Dodoma na kujeruhiwa vibaya na kukimbizwa katika Hosiptali ya Mkoa wa
Dodoma.
CHADEMA tunalaani vikali kitendo hicho, na tunafuatilia kwa karibu hali yake.
Taarifa zaidi zitaendelea kutolewa.
Imetolewa na Kurugenzi ya Uenezi, Mawasiliano na Mahusiano ya Nje.
CHADEMA MAKAO MAKUU
DAR ES SALAAM.
No comments:
Post a Comment