Je, unaamini kwamba kuna uchawi? Asubuhi ya Jumanne wakazi wa jiji la Mombasa walishuhudia sarakasi iliyojumuisha watu wawili waliokuwa uchi wa mnyama.
Wawili hao, mmoja aliyekuwa amembeba nyoka shingoni, walisemekana kuwa walirogwa baada ya kuiba gari la mwanamke mmoja.
Walikuwa wakicheza na kulizunguka gari walioladaiwa kuiba, wakati mwingine wakichota maji ya mvua kwa kutumia nguo zao na kujaribu kuliosha.
Mara kwa mara, wenyewe walichota maji machafu kando ya barabara na kujaribu ‘kuoga’ nayo.
Habari za kisa hicho zilienea sana kwenye mtandao ya kijamii Kenya.
Mchawi aliyedai kuwaroga ilidaiwa alikuwa anaitisha dola 1000 za Marekani kuwazindua.
Lakini baadaye polisi walisema kuwa walikuwa matapeli na kwamba kisa hicho chote kilikuwa kimeigizwa.
Waliwatia mbaroni wahusika wote wanne: wanaume waliokuwa utupu, mwanamke aliyedaiwa kumiliki gari lililoibwa na mwanamke aliyedai kuwa mchawi.
Kwa sababu ya kuwa na nyoka, mchawi alishtakiwa pia na kosa la kumiliki nyara za serikali bila leseni. Wanaume hao wawili walipelekwa kupimwa akili huku mwanamke aliyekuwa amedai gari lake liliibiwa akishtakiwa kosa la kutoa habari za kupotosha kwa maafisa wa polisi
No comments:
Post a Comment