Baada ya taarifa kuzagaa kwenye mitandao ya kijamii kutoka kwa ndugu kwamba mtayarishaji wa muziki kutoka THT, Ema The Boy amepotea na ana siku ya tano hajaonekana, Producer huyo ameibuka kupitia mtandao wa Instagram na kueleza kilichomsibu.
Kupitia taarifa hiyo aliyoitoa kupitia mitandao ya kijamii, Ema alisema alikuwa Bagamoyo kikazi na ameomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza kwa ndugu jamaa na marafiki.
Napenda kuchukua nafasi hii kuwajulisha ndugu jamaa na marafiki wote waliokuwa na wasiwasi juu yangu, ukweli ni kwamba nilikuwa Bagamoyo kikazi zangu binafsi, naomba radhi kwa familia, ofisini, na wadau wote kwa usumbufu uliojitokeza
Niko salama na mzima wa Afya .
Ahsanteni.
No comments:
Post a Comment