Katika mara 7 ambazo Real Madrid wameenda kukipiga Ujerumani
jana ilikuwa mara yao ya kwanza kupata ushind, Cristiano Ronaldo
alifunga mara mbili huku Gareth Bale akifunga lingine katika ushindi wa
mabao 3 kwa 1.
Mengi yameongelewa lakini takwimu zinaonesha Ronnaldo amekuwa striker
ambaye hashikiki haswa linapokuja suala la champions league na namba
zinaonekana wazi jinsi Mreno huyu alivyo na urafiki na nyavu.
Katika michezo 400 ambayo Ronaldo ameichezea Real Madrid mshambuliaji
huyu amewapa Madrid mabao 4111 huku kati ya hayo akifunga hat trick 42.
Cristiano Ronaldo ameshapiga assist 112 huku akiweka kabatini jumla
ya makombe 13 toka ajiunge na Real Madrid, rekodi inayoonesha wazi jinsi
gani pamoja na miaka yake 31 lakini ni mpiga kazi haswa.
Katila Champions League huko ndiko hakamatiki kabisa kwani idadi ya
mabao aliyofunga ni kubwa kuliko michezo aliyocheza, ameweka kambani
mara 93 hiyo ikiwa pungufu ya michezo mitatu aliyocheza(amecheza 90).
Kingine ambacho kinatisha zaidi ni kwamba Ronaldo amehusika katika
mabao 513 ya Real Madrid waliyofunga, huki akifunga mara 14 katika
michezo 9 waliyocheza Champions League mwaka huu.
Lakini je unajua kwamba mashuti 6 kati ya 7 ya mwisho ambayo Ronaldo
aliyapiga langoni mwa wapinzani katika Champions League yalikwenda moja
kwa moja nyavuni na ni moja tu ambalo lilizuiliwa.
Wednesday 27 September 2017
Home
michezo
je kwa rekodi hizi hapa Cristiano Ronaldo anaweza kuwa mchezaji hatari kuwahi kutokea duniani nini?
je kwa rekodi hizi hapa Cristiano Ronaldo anaweza kuwa mchezaji hatari kuwahi kutokea duniani nini?
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Author Details
olger tz ni blog ya kuhusu habari zote za ulimwenguni hapa utaelimika utaburudika na kunufaika na mambo mbalimbali ! ungana nasi kwa habari za kitaifa,kimataifa ,michezo bila ya kusahau habari za wasanii ,visa na mikasa na kadharika!!
No comments:
Post a Comment