Razak Abalora ni Goli kipa ambae ajaruhusu goli mechi 4 za ligi - Olgertz
TANGAZA NASI HAPA

Breaking News

Home Top Ad

TANGAZA NASI HAPA

Wednesday 27 September 2017

Razak Abalora ni Goli kipa ambae ajaruhusu goli mechi 4 za ligi


Razak Abalora ndio golikipa pekee ambaye hajaruhusu goli hadi sasa ikiwa timu zote zimeshacheza mechi nne hadi sasa tangu kuanza kwa ligi.
Golikipa huyo wa Azam amecheza mechi zote nne za ligi kwa dakika 90 kwa kila mechi (sawa na dakika 360) lakini amefanikiwa kuliweka goli lake salama kwa dakika zote hizo.
Alicheza mechi yake ya kwanza VPL wakati Azam ilipopata ushindi wa 1-0 ugenini dhidi ya Ndanda siku ya ufunguzi wa ligi kuu Tanzania bara msimu huu.
Akaendelea kuaminiwa na benchi la ufundi na kucheza mechi dhidi ya Simba iliyomalizika 0-0, Azam ikashinda 1-0 dhidi ya Kagera Sugar kabla ya kushinda tena 1-0 dhidi ya Lipuli huku golikipa huyo raia wa Ghana akiwa langoni.
Golikipa wa Simba Aishi Manula alikuwa akifukuzana na Razakkucheza bila kufungwa lakini Mbao walitibua rekodi yake baada ya kumtungua mabao mawili Simba ilipolazimishwa sare ya kufungana 2-2 uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

No comments:

Post a Comment