MAHAKAMA ya Hakimu ya Mkazi Kisutu,
imepanga Oktoba 6, mwaka huu kutoa hukumu katika kesi ya dawa za
kulevya inayomkabili Yusuf Manji (41).
Uamuzi huo umetolewa jana na Hakimu
Mkazi Mfawidhi, Cyprian Mkeha, baada ya wakili wa utetezi Hajra Mungula
kusema kuwa ameshafunga ushahidi wa mashahidi saba.
Mashahidi watatu wa upande wa
mashtaka wametoa ushahidi wao dhidi ya mshtakiwa Daktari Mfawidhi wa
Gereza la Keko, Inspekta Eliud Mwakawanga ameileza Mahakama ya Hakimu
Mkazi Kisutu jinsi maisha ya mfanyabiashara Yusufu Manji yalivyo kuwa
gerezani kwamba alikuwa akitumia vidonge kati ya 25 mpaka 30 kwasiku.
Alieleza kwamba walikuwa wakimpatia
dawa hizo alipokuwa akisikia maumivu hasa ya mgongo na kwamba kuna
kipindi alikuwa anaamka akiwa na hali ya kutetemeka au kuchanganyikiwa.
Alisema kuwa Julai 6, 2017 walimpokea
Manjia kitokea Hospitali ya Muhimbili Kitengo cha Moyo cha JKCI ambapo
waliambiwa ni mshtakiwa lakini ni mgonjwa.
“Nilienda kumuona, tukazungumza naye na tulikaa naye gerezani hadi alipokuja kuachiwa,”
No comments:
Post a Comment