Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF, Mhe. Seif Sharif Hamad jana
Septemba 26, 2017 ameingia jijini Nairobi Kenya kwenda kumjulia hali
Mbunge wa Singida Mashariki na Rais wa Chama Cha Wanasheria Tanganyika
(TLS), Tundu Lissu ambaye alipigwa risasi.
Mwenyekiti wa kamati ya muda ya uongozi CUF, Julius Mtatiro
amethibitisha hilo na kusema kuwa kiongozi huyo na baadhi ya viongozi wa
CUF wamewasili nchini Kenya kwa ajili ya kwenda kumuona Tundu Lissu.
“Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF, Mhe. Seif Sharif Hamad
ameingia jijini Nairobi kumjulia hali Mbunge wa Singida Mashariki na
Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika Mhe. Tundu Antipas Lisu (leo)
ambaye amelazwa Hospitali ya Nairobi” alisema Julius Mtatiro
Mhe. Shariff Hamad ameongozana na Mhe. Juma Duni Haji Nairobi kumjulia hali, Mhe Tundu Lissu.
Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu alishambuliwa kwa risasi na
watu wasiojulikana Septemba 7, 2017 mjini Dodoma na kisha baadaye
kupelekwa nchini Kenya kwa matibabu zaidi
No comments:
Post a Comment