manji akipanda kwenye gari
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuachia huru Mfanyabiashara Yusufali
Manji (41) na wenzake watatu waliokuwa wakikabiliwa na mashtaka saba ya
uhujumu uchumi na usalama wa Taifa kwa kukutwa na vitambaa
vinavyotengeneza sare za Jeshi la Wananchi wa Tanzania vyenye thamani ya
zaidi ya Sh 200 milioni na mihuri.
Mbali na Manji wengine walioachiwa huru ni Deogratius Kisinda(28), Abdallah Sangey(46) na Thobias Fwere (43).
Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi leo Alhamisi amewaachia huru washtakiwa
hao saa saba mchana mara baada ya Wakili wa Serikali Mwandamizi,
Kishenyi Mutalemwa kuomba ifutwe kwa kuwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP)
hana nia ya kuendeleza mashtaka hayo dhidi ya washtakiwa hao na
Mahakama ikaridhia.
Akiwasilisha ombi hilo mahakamani hapo, Wakili Kishenyi amesema kuwa leo
yaani siyo tarehe ya kesi hiyo, ila waliomba hati ya wito ya mshtakiwa
(Remove order) na kuiarifu Mahakama kuwa DPP kwa niaba ya jamuhuri
hakusudii kuendelea kuwashtaki washtakiwa hao katika kesi hiyo na
akaomba iondolewe chini ya kifungu cha 91 (1) cha Sheria ya Makosa ya
Jinai (CPA) Sura ya 20.
Baada ya kueleza hayo, Wakili wa washtakiwa hao, Hajra Mungula aliusema
sheria hiyo inaruhusu DPP kuwaachia huru washtakiwa na pia inaruhusu
kuwakamata.
Hakimu Shaidi kutokana na ombi hilo, aliwaambia washtakiwa hao kuwa mashtaka yamefutwa, wako huru hivyo waondoke.
Mara baada ya kuachiwa huru, Manji aliulizia kuhusu malalamiko yake
aliyoyawasilisha mahakamani hapo kuhusu udiwani wake na Hakimu Shaidi
alimueleza kwa kuwa yuko huru atalishughulikia hilo.
Manji alishaeleza kuhusiana na kutokubaliana na hatua ya kumvua udiwani iliyofikiwa na halmashauri ya manispaa.
Baada ya kuelezwa hayo Manji na wenzake waliondoka kwa kutumia gari moja
mahakamani hapo kuelekea nyumbani kwao. Kesi hiyo kabla ya kufutwa
ilikuwa katika hatua ambayo upelelezi wake ulikuwa bado haujakamilika
na ilipangwa kutajwa mahakamani hapo Septemba 18,2017.
Kwa mara ya kwanza kesi hiyo, ilisomwa Julai 15, 2017, katika Hospitali
ya Taifa ya Muhimbili kwenye Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete ambapo
Manji alikuwa amelazwa kutokana na matatizo ya moyo.
Kesi hiyo ilisomwa siku hiyo na wakili wa serikali Tulumanywa Majigo
ambaye alidai kuwa Juni 30, 2017 katika eneo la Chang’ombe ‘A’wilaya ya
Temeke Dar es Salaam washtakiwa hao kwa pamoja walikutwa na askari
polisi wakiwa na bunda 35 za vitambaa vinavyotumika kutengenezea sare za
Jeshi la Wananchi Tanzania zenye thamani ya Sh 192.5milioni na kwamba
mali hiyoilipatikana kinyume cha sheria.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Author Details
olger tz ni blog ya kuhusu habari zote za ulimwenguni hapa utaelimika utaburudika na kunufaika na mambo mbalimbali ! ungana nasi kwa habari za kitaifa,kimataifa ,michezo bila ya kusahau habari za wasanii ,visa na mikasa na kadharika!!
No comments:
Post a Comment