Jaji mmoja nchini Marekani
amemuhukumu kifungo jela aliyekuwa muuzaji dawa Martin Pharma Bro
Shkreli akisubiri hukumu ya kusababisha hofu ya kiusalama.
Jaji
Kiyo Matsumoto alisema kuwa chapisho la mtandao wa facebok ambalo
Shkreli aliahidi kumzawadi mtu yeyote atakayempatia unywele wa Hillary
Clinton lilionyesha kuwa ni hatari kwa umma.Shkreli aliyewahi kuwa afisa mtendaji wa zamani amekuwa huru baada ya kutoa dhamana ya dola milioni tano tangu alipokamatwa 2015.
Shkreli alitajwa kuwa mtu anayechukiwa zaidi nchini Marekani baada ya kampuni yake ya kuuza dawa kuongeza bei ya dawa zinazotumiwa na wagonjwa wa Ukimwi.
Mnamo mwezi Agosti 2017 alipatikana na hatia ya makosa matatu kuhusiana na usalama na jopo la majaji ambalo pia lilifutilia mbali makosa mengine matano dhidi yake.
Shkreli alikuwa ameshtakiwa kuhusiana na kampuni ya dawa aliyomiliki Retropin mbali na hazina aliyokuwa akisimamia.
Siku ya Jumatano, Jaji Matsumoto aliamua kwamba chapisho hilo la Shkreli mnamo tarehe nne mwezi Septemba lililowekwa muda mfupi kabla ya bi Clinton kuanza ziara yake ya vitabu, lilionyesha kuwa ni hatari akikana hoja ya Shkreli kwamba maneno yake yalilindwa na uhuru wa kujieleza.
Shkreli ambaye amekuwa akisuguana na wakosoaji wake katika mitandao ya kijamii alidai kwamba chapisho hilo lilikuwa la kejeli na la mpangilio wa DNA.
''Hili ni ombi lililochapishwa kwa lengo la kuwazawadi watakaokuletea unywele huo'', alisema jaji huyo.
Wakili wa Shkreli Benjamin Brafmin alisema: Tumekatishwa tamaa.Tunaamini kwamba mahakama ilifanya uamuzi wa makosa .
''Lakini yeye ni jaji na sasa tutalazimika kukubali uamuzi huo'
No comments:
Post a Comment