Mkali wa 'Seduce Me' Ally Salehe Kiba, amefunguka na kusema katu hataweza kuishi maisha ya kuigiza umaarufu kwani anaamini watu ndiyo waliompokea kipindi akiwa hana kitu hivyo kujikweza ni kuwatengenezea watu hao hila mioyoni mwao.
Kiba alifunguka hayo wakati akitoa ushauri kwa wasanii wachanga kwa kuwaambia kwamba hakuna kitu kibaya kama kuishi maisha ya kuigiza umaarufu kwani yanakuwa siyo maisha yao halisi.
"Watu wanashindwa kujua kuwa umaarufu wamepatiwa na watu ambao ni mashabiki zetu sisi. Sasa kuwa na pesa haimaanishi kuwa uishi kwa kuwakomesha waliokuweka hapo, usiiishi kwa kuwatengenezea watu hila mioyoni mwao. Kwanz hakuna mtu mwenye pesa. Pesa zote tunazotamba nazo ni za serikali hivyo mtu anayejifanya kwamba anapesa azifungie ndani aone jinsi ambavyo maisha yatakuwa. Hata masuala ya kuvimba ni ya kuacha kwani najua tukipata majanga tutaungana tu."
Alikiba aliongeza kuwa "Mimi nikisema niishi kistaa ukweli sijui itakuaje, lakini kwa vile naamini mimi ni Super Star hivyo siwezi ku-act maisha kwa vile naamini yale siyo maisha yangu, ingawa wapo watu wengi ambao wanaigiza maisha hayo. Naamini kuwa kuna watu wanafanya kufurahisha mioyo yao. Lakini kama ni umaarufu Mzee Majuto mwenyewe ni Star lakini anaishi maisha ya kawaida sana, maisha ya umaarufu siyo ya kwetu tujaribu kuishi maisha yetu ya kitanzania.
Akiwaasa wasanii wachanga Kiba amewataka wasanii hao wajifunze kupitia wakongwe wa zamani kwa jinsi ambavyo walikuwa wakiishi kwa upendo ikiwa ni pamoja na kusapotiana kwa kuonyeshana upendo na kushikana mikono.
"Natamani kuona jinsi ambavyo wasanii wa zamani walivyokuwa wakisapotiana ndivyo iwe kwa wasanii wa sasa. Mimi ni mkongwe lakini kuna wakongwe zaidi niliowakuta na hatukua na sapoti ya mitandao lakini love ya kutosha ilikuwepo. Wasanii wa sasa wanaigiza kuishi ki-staa pamoja na kuvimbiana kwa upande wangu ningewataka waache kuvimba na waweke nguvu kwenye kazi pamoja na heshima" Alikiba
No comments:
Post a Comment