Ameeleza kuwa kwa sasa Serikali imejitahidi kuongeza upatikanaji wa dawa na imeamua kuanza kununua dawa kutoka kwa wazalishaji badala ya kununua kutoka kwa wafanyabiashara kama ilivyokuwa awali.
>>>”Watendaji badala ya kuwaandikia wagonjwa dawa zilizo kwenye orodha, wanaandika dawa zao na kuwaambia wagonjwa wakanunue dawa kwenye maduka ya dawa. Hatukatazi Watumishi kuwa na maduka ya dawa ila muhimu kuchora mstari wa dawa za Serikali na dawa ambazo sio za Serikali.” – Waziri Ummy Mwalimu.
No comments:
Post a Comment