Kylian Mbappe alitamani zaidi kuichezea Arsenal na sio timu nyingine - Olgertz
TANGAZA NASI HAPA

Breaking News

Home Top Ad

TANGAZA NASI HAPA

Wednesday, 6 September 2017

Kylian Mbappe alitamani zaidi kuichezea Arsenal na sio timu nyingine


Kylian Mbappe kwa mara ya kwanza hii leo amefika katika uwanja wa mazoezi wa klabu yake mpya ya PSG ili kujiandaa na michezo ya ligi kuu nchini Ufaransa inayotarajiwa kuendelea wikiendi hii.
Wakati wa dirisha la usajili Mbappe alihusishwa na kwenda katika vilabu vingi kama vile Real Madrid, Manchester City na Arsenal pia walikuwa kwenye mbio za kumnasa Mfaransa huyo lakini alitua PSG.
Hii leo Kylian Mbappe ameongea na gazeti moja la michezo na kati ya mambo aliyosema ni kwamba alikutana na kocha Arsene Wenger na kutokana na heshima ya kocha huyo nchini Ufaransa angejiunga Arsena.
Ndio nilikutana na Arsene Wenger ambaye ni kocha mkubwa, ana heshima kubwa hapa Ufaransa na anajua kuendeleza vipaji vya wachezaji vijana nilipendezwa kwenda Arsenal” alisema Mbappe
Hata hivyo iko wazi kwamba ni ngumu kwa Arsenal kutoa kiasi cha pesa kama walichotoa PSG, sasa Mbappe anaenda kutengeneza utatu wa hatari PSG akicheza pamoja na Edson Cavanni na Neymar Dos Dantos.

No comments:

Post a Comment