Nguli wa Muziki wa country Afariki dunia ni Don Williams - Olgertz
TANGAZA NASI HAPA

Breaking News

Home Top Ad

TANGAZA NASI HAPA

Friday 8 September 2017

Nguli wa Muziki wa country Afariki dunia ni Don Williams

Don Williams. Photo: September 1979Don Williams alianza kuimba muziki kama mwanamuziki wa kujitegemea mwaka 1971

Mwanamuziki nyota wa nyimbo za mtindo wa country kutoka Marekani Don Williams amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 78.
Mzaliwa huyo wa jimbo la Texas amefariki baada ya kuugua kwa muda mfupi, afisa anayesimamia mawasiliano yake ametangaza.
Williams alianza kuimba nyimbo kama mwanamuziki wa kujitegemea mwaka 1971, na tangu wakati huo alichomoa nyimbo 17 zilizogonga chati za muziki wa country.
Nyimbo zake zilizovuma zaidi ni pamoja na Gypsy Woman na Tulsa Time, ambazo ziliimbwa tena na wanamuziki wengine kama vile Eric Clapton na Pete Townshend. Williams alitazamwa na wengi kama gwiji mnyenyekevu wa muziki wa country.
Nyimbo zake nyingine zilizovuma ni pamoja na You're My Best Friend, I Believe in You na Lord, I Hope This Day Is Good

No comments:

Post a Comment