Phellipe Coutinho uhamisho wake kwenda Barcelona umeshindikana, inafahamika wazi kwamba Coutinho aliomba kuuzwa kwenda kukipiga na Barcelona lakini klabu ya Liverpool ilibana.
Tangu sakata la usajili la Coutinho litokee amekuwa nje ya uwanja lakini majuzi wakati wa michezo ya kufudhu kwa fainali za kombe la dunia Coutinho aliliwakilisha taifa lake la Brazil na alionekana fiti.
Michezo ya kufudhu fainali za kombe la dunia imemalizika na wikiendi hii ligi kuu nchini Uingereza Epl inaendelea huku Liverpool wakikipiga dhidi ya Manchester City lakini Coutinho hatakuwepo katika mchezo huo.
Jurgen Klopp amethibitisha kwamba hajamjumuisha Phellipe katika kikosi hicho ili kuzidi kumpa muda wa kupumzika lakini amesema kiungo huyo wa Kibrazil ameafiki suala hilo.
“Nilishaongea naye, tuna michezo saba katika wiki tati zijazo na kutakuwa na muda mchache sana wa kufanya mazoezi, kabla hajaenda Brazil alikuwa hajafanya mazoezi na ni vyema kumpa muda wa kutosha kwa ajili ya msimu” alisema Klopp.
Lakini Klopp amesema kutokana na yaliyotokea wakati wa usajili Coutinho ameshayasahau na amekubaliana na kila kilichotokea kwa 100% na sasa yuko tayari kwa ajili ya kuipigania klabu yake ya Liverpool
No comments:
Post a Comment