Gari la Mh tundu Lissu likiwa na matobo ya Risasi
Mbunge wa Rombo, Joseph Selasini ameeleza jinsi Mbunge wa Singida
Mashariki, Tundu Lissu alivyopigwa risasi nyumbani kwake mjini Dodoma.
Selasini amesema kuwa maelezo aliyopata ni kuwa alikuwa akifuatiliwa na
gari tangu anatoka bungeni na dereva wake alilishtukia.
Amesema kuwa alivyoona wanamfutilia alipofika nyumbani, dereva alimsihi Lissu asishuke ndani ya gari.
"Hao watu walipoona hawashuki walijifanya kuna kitu wanaangalia
walivyoona kuna utulivu walisogeza gari lao ambalo ni tinted na kuanza
kurusha risasi upande wa Lissu." amesema
Selasini amesema, “Risasi zilimpata mguuni, mkononi na tumboni lakini daktari anasema anaendelea vizuri."
Lissu amepigwa risasi leo Alhamisi na kupelekwa chumba cha upasuaji katika Hospitali ya Rufaa ya Dodoma
Pichani: Mh Joseph Selasini
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Author Details
olger tz ni blog ya kuhusu habari zote za ulimwenguni hapa utaelimika utaburudika na kunufaika na mambo mbalimbali ! ungana nasi kwa habari za kitaifa,kimataifa ,michezo bila ya kusahau habari za wasanii ,visa na mikasa na kadharika!!
No comments:
Post a Comment