Mchezo wa Hertha Berlin dhidi ya Werder Bremen wa Bundesliga uliyochezwa leo na kumalizika kwa sare ya 1-1, ulichezeshwa na Bibiana Steinhaus ambaye nje ya urefa ni askari Polisi, mchezo wa leo ndio mkubwa wa wanaume aliyowahi kuuchezesha.
Bibiana ameanza kazi ya uamuzi toka mwaka 2007 hadi kufikia hapo amechezesha michezo zaidi ya 80 ya Ligi daraja la pili, amechezesha fainali ya wanawake ya Champions League 2017 na michuano ya wanawake ya Olympic 2012 London lakini tegemea kuendelea kumuona Bundesliga wa 2017/2018 akichezesha mechi kadhaa
No comments:
Post a Comment