PICHA : Mc Gregor baada ya kufumuliwa na Floyd Mayweather asaivi anakula Bata si la kitoto - Olgertz
TANGAZA NASI HAPA

Breaking News

Home Top Ad

TANGAZA NASI HAPA

Sunday, 10 September 2017

PICHA : Mc Gregor baada ya kufumuliwa na Floyd Mayweather asaivi anakula Bata si la kitoto

Usiku wa August 27 2017 Bondia mwenye sifa ya kutopoteza pambano hata moja Floyd Mayweather alirudi ulingoni kucheza pambano la 50 dhidi ya Mc Gregor hiyo ikiwa ni muda umepita toka apigane na Manny Pacquiao na kumpiga.

Mc Gregor ambaye alionekana kuwa na tambo alipigwa na Mayweather kwa Technical Knock Out (TKO) round ya 10 pambano la round 12, huo ukawa ni mwisho wa tambo zake dhidi ya Mayweather, licha ya kipigo hicho Mc Gregor kupanda tu ulingoni kulimfanya aingize dola milioni 100 ambazo ni zaidi ya Tsh bilioni 200 za kitanzania.

 Mc Gregor anayetokea Ireland ameonekana akiwa amekodi boti binafsi akiwa na familia yake wanaendelea kula bata Hispania katika fukwe za Ibiza, kitu ambacho wengi wanaamini anatumia au ana furaha kuingiza Dola milioni 100 licha ya kupoteza.



Mc Gregor na Mayweather walipopambana

No comments:

Post a Comment