
Kumeshuhudiwa msongamano mkubwa wa magari na upungufu wa petroli, wakaazi wa Florida wakielekea maeneo ya kaskazini.
Wakati huo huo kimbunga Ema kinachoendelea kusonga kwa kasi,sasa kimeingia nchini Cuba.
Kimbunga hicho, kinaandamana na upepo mkali na mvua kubwa kuelekea visiwa vya kaskazi mwa Caribbean.
Bahamas hata hivyo imenusurika na kimbunga hicho baada ya upepo kubadilisha mkondo. Visiwa vya mashariki vilivyokuwa vimekumbwa na
mafuriko makubwa sasa ya yanakabiliwa na tishio la kugongwa na kimbunga kingine.
Shughuli ya kuwaondoa watu katika kisiwa cha Barbuda ilikamilika.
No comments:
Post a Comment