Nuhu Mziwanda:Ndoa yangu ilivunjika chanzo ni Wazazi - Olgertz
TANGAZA NASI HAPA

Breaking News

Home Top Ad

TANGAZA NASI HAPA

Friday 29 September 2017

Nuhu Mziwanda:Ndoa yangu ilivunjika chanzo ni Wazazi

Image result for Nuh Mziwanda picture
Mwanamuziki Nuh Mziwanda amekanusha suala linaloongelewa na watu kuwa kuvunjika kwa mapenzi kati yake na mzazi mwenzie chanzo chake siyo Shilole bali ni wazazi wa binti huyo.

“Unajua watanzania ukiwapa picha tu, basi wao wataandika maneno wataandika wenyewe Shilole hausiki hata kidogo kuvunjika kwa mahusiano yangu.”Image result for Shilole

“Wahusika ni wazazi wake ambae yeye aliamua kuwasikiliza wazazi wake kwa kuolewa na mtu mwingine na hatukuwa na ugomvi wowote ila ndio hivyo wazazi walikuwa na nguvu sana kunizidi mimi,” aliongeza.

Aidha Nuh Mziwanda aliongeza kuwa mahusiano yake ameyaweka kando na yupo kupambana na hali yake, lakini anashukuru Mungu mtoto wake bado anaendelea vizuri na anapata taarifa zote muhimu kumuhusu mtoto wake lakini mengine imebaki stori.

No comments:

Post a Comment