TFF Yaanika Viingilio Mechi ya Tanzanite Dhidi ya Nigeria - Olgertz
TANGAZA NASI HAPA

Breaking News

Home Top Ad

TANGAZA NASI HAPA

Friday 29 September 2017

TFF Yaanika Viingilio Mechi ya Tanzanite Dhidi ya Nigeria

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEj4HYdGWtU38DtP91jzrM_3eFfOW0uKmNfpXUx5T_w8AIFd7axYFEArKPUBQN5yJ9s_zJkocMIXhEDxdl9XHyAlTPo8X8LoSMA-6sm-OQgdkKtBkJeUVhRBpZ-KKsAAO9_8olgXahRBlIk/s1600/Nembo-ya-TFF.jpg
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeweka wazi viingilio vya mchezo wa marejeano kuwania kufuzu fainali za Kombe la Dunia dhidi ya Nigeria itakayopigwa, Jumapili Oktoba mosi, mwaka huu.

Mashabiki wataingia kwenye uwanja wa Azam Complex kwa viingilio vya kawaida kushuhudia mechi hiyo timu ya taifa ya wanawake wenye umri wa chini ya miaka 20 ‘Tanzanite’ itakayocheza dhidi ya Falconets ya Nigeria.

Viingilio vitakuwa ni Sh. 5000 tu kwa mashabiki watakaoketi eneo la mzunguko huku kwa wale watakaokaa jukwaa kuu (VIP) watalipia Sh. 1,0000 tu katika mchezo utakaofanyika Uwanja wa Azam, Chamazi ulioko nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.

Kocha wa Tanzanite, Sebastian Nkoma, amesema kwa namna alivyokiandaa kikosi chake ana imani kitaweza kupindua matokeo ya awali ambayo Tanzanite ililala mabao 3-0 katika mchezo uliofanyika Uwanja wa Samuel Ogbemudian, ulioko Jimbo la Benin nchini Nigeria, wiki mbili zilizopita.

No comments:

Post a Comment