Msanii wa muziki wa kizazi kipya Khalid Mohamed maarufu kama T.I.D, ametangaza nia ya kugombea ubunge jimbo la Kinondoni, kwenye uchaguzi ujao unaotarajiwa kufanyika mwaka 2020, na kumng’oa mbunge wa sasa wa jimbo hilo Maulid Mtulia.
Akizungumza na redio moja hapa nchini, TID amesema sababu inayomsukuma kugombea nafasi hiyo ni kutokana na mbunge wa sasa kushindwa kulitimizia mahitaji yake jimbo hilo, hivyo atatumia nafasi hiyo kuhakikisha anamng’oa ifikapo 2020, kwa kuwa yeye anafahamu vizuri matatizo ya Kinondoni kutokana na kuwa mzawa wa mahali hapo.
Akiendelea kuzungumzia suala hilo, TID amesema iwapo atapewa dhamana ya kuliongoza jimbo hilo, atahakikisha anatatua matatizo yote yanayowakabili watu wa Kinondoni, likiwemo janga la madawa ya kulevya.
No comments:
Post a Comment