Ule msemo wa ‘mwizi siku zake ni arobaini’ asubuhi ya leo August 6, 2017 umedhihirika baada ya vijana wawili wanaoripotiwa kuwa wezi wa gari waliloliiba siku za nyuma kulirudisha gari hilo wakiwa uchi wa mnyama na wakionekana kuwa wamerukwa akili jambo lililokusanya umati wa watu kuwashangaa.
Tukio hili lilitokea kwenye mji wa Bamburu Mtambo huko Mombasa Kenya ambapo vijana hao walifika eneo hilo na gari hilo walilokuwa wameliiba Nissan KBV 717Y ya rangi ya silva na kutoka nje ya gari wakiwa uchi, wakiwa wanaongea lugha isiyoeleweka na baadae kuanza kuosha gari hilo kwa matope kabla ya wao kuanza kujipaka matope hayo.
Wakazi wa eneo hilo wameeleza kuwa wanaamini mmiliki wa gari hilo alikwenda kwa mganga wa kienyeji na kuwaroga watu hao kutokana na kuliiba gari lake.
No comments:
Post a Comment