Klabu ya Barcelona wanaonekana hawataki kuelewa kauli za
Jurgen Klopp kwamba Phellipe Coutinho hauzwi na hakuna dau lolote
linaloweza kumng’oa kutoka Anfield, baada ya dau la kwanza la euro 80m
kukataliwa sasa Barca wanaenda kuongeza 20 zingine kumnasa Coutinho.
Habari nyingine za usajili ni kwamba baada ya Manchester United
kumkosa Eric Dier sasa klabu ya Bayern Munich inajiandaa kuwajaribu
Tottenham Hotspur kwa kumnunua kiungo huyo huku wakiwa na kiasi cha euro
55m katika begi lao.
Katika kuendelea kuhakikisha kwamba wanarudisha heshima ndani ya
klabu yao, Ac Millan wanajipanga kumrudisha Zlatan Ibrahimovich huku
wakala wake Massimo Mirabelli akikiri uwezekano wa kutikea jambo hilo.
Baada ya tetesi nyingi sana kuhusu kuondoka kwake sasa mshambuliaji
wa Arsenal Alexis Sanchez anaonekana kukubali kubaki katika klabu yake
ya Arsenal huku akiangalia mustakabali wa maisha mengine ndani ya klabu
hiyo.
Baada ya kipigo kutoka Arsenal katika mchezo wa ngao ya hisani sasa
kocha wa Chelsea Antonio Conte anataka kusajili wachezaji wengine huku
jina la mlinzi Virgil Van Dijik likiongoza orodha ya wachezaji
wanaohitajika darajani
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Author Details
olger tz ni blog ya kuhusu habari zote za ulimwenguni hapa utaelimika utaburudika na kunufaika na mambo mbalimbali ! ungana nasi kwa habari za kitaifa,kimataifa ,michezo bila ya kusahau habari za wasanii ,visa na mikasa na kadharika!!
No comments:
Post a Comment