LICHA ya kusambaa video yake ya zamani akielezea anavyompenda msanii wa Bongo Fleva, Barakah The Prince huku akionesha tattoo aliyojichora jina lake, staa wa sinema za Kibongo, Salma Jabu ‘Nisha’ ameibuka na kufunguka kuwa mpenzi wake wa sasa hafurukuti kwani anamwamini vilivyo.
Akizungumza na Ijumaa Wikienda, Nisha alisema kuwa, licha ya watu kutaka kumuharibia kwa mpenzi wake huyo aliyemtaja kwa jina moja la Minu kwa kurusha mitandaoni video za wapenzi wa zamani, hawawezi kumuachanisha naye kwa sababu mwanaume wake huyo anamwamini.
“Hiyo video ya Barakah ni ya zamani sana, lakini ninaona watu wameiweka ili waniharibie kwa Minu, jambo ambalo haliwezekani kwani ananiamini na yuko peke yake kwangu, nami niko peke yangu kwake,” alisema Nisha.
Source : Ijumaa wikienda
No comments:
Post a Comment