Nyota wa filamu za Hollyhood, Angelina Jolie, amekuwa na wakati mgumu tangu alipoachana na mpenzi wake Brad Pitt mwaka jana.
Aliambia
Gazeti la Telegraph: ''Nimekuwa na wakati mgumu. Sifurahi kuwa bila
mpenzi. Si jambo nililolitaka. Hakuna kitu chochote kizuri kuhusiana na
hilo. Ni jambo gumu sana.''Katika mahojiano mengine na gazeti la Australia Sydney Morning Herald , alisema ametumia muda wake mwingi mwaka jana , ''nikiwaangalia watoto wangu.''
''Siwezi kujifanya, huu ni wakati mgumu katika maisha yangu,'' aliongeza.
Lakini najaribu kukabiliana na tatizo hili kwa kuzingatia mambo yajayo na kutambua kwamba ni mambo ya kawaida kwa mwanadamu.
''Labda wakati mwengine inaonekana najilimbikizia kila kitu, lakini kwa kweli najikaza kusukuma siku zangu.
''Hatimaye nitaweza kufanya kazi nyingi tofauti kwa wakati mmoja, lakini kutokana na masuala ya kifamilia mambo yamekuwa magumu zaidi picha ya pamoja na Brad Pitt Aliyekuwa mumewe Angelina Jolie
No comments:
Post a Comment